
Seleman Matola(Kushoto) akiwa na aliyekuwa kocha mkuu wa Simba, Sven Vandenbrock enzi wakifanya kazi pamoja.
Abbas Ally aliyasema hayo alipozungumza na East Africa Radio ikiwa ni siku moja baada ya kuvunjwa kwa kambi ya kikosi chao ambapo wamewapa wiki moja wachezaji kupata mapumziko baada ya mashindano ya Mapinduzi visiwani Zanzibar.
''Tumetoa wiki moja kwa wachezaji kupumzika baaa ya kuwa nao kwa muda mrefu, tuliweka kambi tangu tulipokuwa tunajiandaa na mchezo dhidi ya Plateau United ya Nigeria, na hata tuliporejea hawakupumzika hadi michuano ya Mapinduzi, hivyo tunawapa wiki moja wao na benchi la ufundi na watarejea baada ya wikii moja.
Kuhusu iwapo baada ya wiki moja je Kocha Seleman Matola ndiye atakayeongoza mazoezi au atajiunga na Taifa Stars nchini Cameroon, siwezi kulizungumzia zaidi ya waajili wake na TFF '' Alisema mratibu wa Simba, Abbas Ally.
Ikumbukwe Seleman Matola alikaimishwa mikoba ya Sven Vandenbroeck aliyekuwa kocha mkuu wa wekundu hao ambaye aliondoka na kujiunga na FAR Rabbat ya Morocco, ikiwa ni muda mchache baada ya kuwawezesha mabingwa hao wa Tanzania bara kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika.