Sunday , 17th Jan , 2021

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya ametoa wito kwa wafanyabiashara kujenga viwanda vya mbolea ili izalishwe kwa wingi hapa nchini na kusaidia bei ishuke kwa manufaa ya wakulima.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya

Kusaya ametoa rai hiyo wilayani Kilombero alipoongea na wakulima kufuatia malalamiko ya kuuziwa mbolea kwa bei kubwa.

"Ni nafasi yetu kutoa wito kwa wafanyabiashara, kwa mtu yoyote ambaye anaweza kuwekeza kwenye suala zima la viwanda vya mbolea, tunawashawishi pamoja na biashara wanazofanya pia wafungue na viwanda vya mbolea serikali imetengeneza mazingira rafiki" amesema Kusaya

Aidha Kusaya amesema kuwa mbolea nyingi in atoms nje kutokana na changamoto hii ya kukosekana kwa viwanda vikubwa vya mbolea hapa nchini