Tuesday , 2nd Feb , 2021

Kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli aliposimama wilayani Manyoni Jumapili Jan 31, 2021 na kusikiliza kero ya Bi. Elizabeth Msalala ya kuporwa ardhi yake, sasa amerejeshewa haki zake.

Rais Magufuli (kushoto) na Bi. Elizabeth Msalali (kulia)

Katika kero hiyo Rais Magufuli alibaini kuwa ardhi iliporwa na kupewa aliyekuwa mtumishi wa idara ya ardhi wilayani humo jambo ambalo limemfanya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Eng. Kundo Andrea Mathew kufika eneo hilo.

Akiwa hapo Naibu Waziri ameagiza kusitisha malipo yote yanayotokana na kodi ya mnara wa kampuni ya Helios towers na kuhamishia kwa mmiliki halali wa eneo hilo, ambaye ni Bi Elizabeth Msalala.

Adam Kazimoto ambaye alijitokeza mbele ya Rais kutoa kero hiyo anaishukuru serikali kwa hatua iliyofikia kuanza utekelezaji wa kurudisha umiliki wa eneo hilo akiwemo Bi.Elizabeth Msalali ambaye ndiye anayedaiwa kuwa ni mmiliki halali wa kiwanja hicho.
 

Zaidi Tazama Video hapo chini