
Klabu ya Liverpool hairuhusiwi kuingia nchini Ujerumani kutokana na maambukizi ya Covid- 19 kuongezeka nchini England
Wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani imeiarifu klabu ya RB Leipzig kuwa mchezo dhidi ya Liverpool haujakidhi mahitaji kulingana na kanuni za sasa za kujikinga na virusi vya Corona, mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa klabu bingwa ulaya hatua ya 16 bora umepangwa kuchezwa Februari 16, 2021.
Taifa la Ujerumani limeweka vizuizi kwa baadhi ya wasafiri kuingia nchini humo kutoka kwenye mataifa ambayo yanamaambukizi ya juu ya virusi vya Corona, ambapo England ni moja ya taifa ambalo lipo kwenye orodha hiyo.
hirikisho la soka barani ulaya UEFA liliboresha kanuni zake juu ya janga la Corona, iliweka wazi kuwa kama timu mwenyeji haiwezi kuandaa mchezo kwenye uwanja wake basi inalazimika kutafuta uwanja mwingine ambao watautumia kuandaa michezo yao ya nyumbani, na kama watashindwa basi timu pinzania itapewa alama 3 na ushindi wa mabao 3-0.
Inaripotiwa kuwa uwanja wa Puskas uliopo mjini Budapest nchini Hangary ndio utakao tumika kuandaa mchezo huo kama uwanja wa nyumbani wa Leipzig lakini pia inatajwa mchezo huo unaweza kufanyika kwenye moja ya viwanja nchini England.