Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Halmashauri zitumie fedha kwa utaratibu- Mabula

Sunday , 28th Feb , 2021

Niabu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula ameibana Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kurejesha fedha kiasi cha shilingi milioni 418 ilizopewa na Wizara ya Ardhi kwa ajili ya mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha viwanja katika manispaa hiyo.

Niabu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula

Akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi na wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Iringa katika kikao kazi  Dkt Mabula alisema fedha ilizopewa Manispaa ya Iringa ni mkopo kwa ajili ya kupima viwanja na siyo kwa ajili ya shughuli nyingine za halmashauri.

"Wizara imetoa fedha ili upime viwanja na kuuza na baadaye urudishe fedha lakini ninyi badala ya kurudisha fedha mmetumia kwenye mambo mengine, wenzenu Geita faida waliyopata katika mradi kama huu walinunua gari la idara ya ardhi, hatuwezi kutumia fedha kwa utaratibu huo,’’ alisema Naibu Waziri Mabula.

Waziri Mabula  alizitaka halmashauri zote zilizokopeshwa fedha na Wizara ya Ardhi kwa ajili ya mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha viwanja kuzirejesha kulingana na makubaliano ili kuwezesha halmashauri nyingine zenye uhitaji kukopa. Alisema halmashauri zitakazokaidi kuzirejesha fedha kwa wakati basi suala hilo litawasilishwa mamlaka husika ili wahusika wakatwe fedha hizo moja kwa moja.

Aidha Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa Hamid Njovu alimuahidi Naibu Wzairi wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa halmashauri yake itahakikisha inakamilisha kulipa deni hilo kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha 2020/2021.

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine