
Baby Mama wa Barakah The Prince, mrembo Careen Simba
"Mwanaume kumpa pesa mwanamke ni jukumu lake kwa kweli na kama mwanamke wako lazima umuhudumie ingawa na yeye anatakiwa afanye kazi sio kila kitu mpaka amwambie mwanaume wake, ni jukumu la mwanaume kutoa pesa kwa mwanamke sio kama unamuhonga bali ni kumjali ili asije akaangaliwa na watu wengine mwisho wake akusaliti" ameeleza Careen Simba
Kwa sasa mrembo huyo anaigiza filamu na ametokea kwenye video ya wimbo mpya wa Kala Jeremiah pia amefunguka chanzo cha kuachana na Barakah The Prince alikuwa ni Najdattan.
Mtazame hapa chini kwenye video.