Sunday , 7th Mar , 2021

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, kimemshukuru Jaji wa Mahakama Kuu Dkt. Ntemi Nimilwa Kilikamajenga, kwa kuahidi kuwashughulikia Mawakili watakaolalamikiwa kufanya kazi zao bila weledi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole

Polepile ameibainisha kuwa Jaji Ntemi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mawakili ametoa fursa ya Mawakili wasioweledi kuripotiwa ili wachukuliwe hatua ikiwemo kufutwa wakafanye kazi nyingine.

Aidha Polepole ameeleza kuwa hatua hiyo imekuja kutokana na uwepo wa baadhi ya Mawakili ambao hawatimizi majukumu yao ya kutetea haki kwa watu badala yake hufanya kinyume chake.

Tazama Video hapo chini