Wednesday , 10th Mar , 2021

Migororo ya ndoa imetajwa kuendelea kuongoza katika jamii mkoani Kagera, huku kundi la ndoa zenye umri mfupi hadi miaka mitano likiongoza kwa migogoro na kufuatiwa na kundi la wazee waliostaafu na kupata mafao.

Mratibu wa kitengo cha kusuruhisha migogoro na kutetea haki za binadamu kilichoko chini ya Kanisa la KKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Naomi Kanyonyi

Akizungumzia mwenendo wa vitendo vya ukatili mkoani Kagera, mratibu wa kitengo cha kusuruhisha migogoro na kutetea haki za binadamu kilichoko chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Naomi Kanyonyi, amesema kuwa kwa mwaka 2020 wamepokea jumla ya migororo 797 lakini asilimia kubwa ya migororo hiyo ni ya ndoa.

Mratibu huyo ametaja baadhi ya chanzo cha migogoro katika ndoa kuwa ni kutopata mafundisho ya kutosha kabla ya ndoa na baadhi ya wanandoa kukutana mitandaoni, tofauti na zamani ambapo wanaukoo, familia na wazazi walishiriki kutafuta binti au kijana anayefaa.

Baadhi ya viongozi wa dini akiwamo mchungaji King James, wa kanisa la Adonai Bukoba wamesema kuwa suala hilo linatokana na kukosekana kwa utii na upendo kwa wana ndoa.