
Mshambuliaji wa Chelsea, Olivier Giroud (katikati) akifunga bao la ushindi alipocheza na Atletico Madrid Mchezo uliopita.
Mchezo wa Cheslea dhidi ya Atletico Madrid inatazamiwa kuwa wenye upinzani mkali kutokana kocha wa Atletico Madrid kusema kuwa mchezo huo bado haujaisha na wananafasi ya kufanya vizuri na kupindua matokeo hayo.
Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel ambaye hajapoteza mchezo hadi hivi sasa tokea ajiunge na matajiri hao wa jiji la London mwishoni mwa mwezi Januari, ameshinda michezo 8 na kusare 4, amekiri kuwa mchezo huo utakuwa ni wa kukata na shoka hivyo watapambana kupata ushindi ili kusonga hatua inayofuata.
Kwa upande wa timu wenyeji, Klabu ya Chelsea, inataraji kuwakosa mlinzi wake tegemezi, Thiago Silva na mshambuliaji Tamy Abraham wenye majeraha ilhali kiungo Mason Mount na Jorginho watakosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kukosa mchezo kufuatia kuonesha kadi za njano 2.
Atletico Madrid wamethibitisha kutokuwa na wachezaji wenye majeraha ya hvi karibu na badala yake beki kitasa Jose Maria Gimenez, kiungo Yannick Carrasco na mlinzi wa kulia Kieran Trippier wamerejea kikosini.
Hii itakuwa ni mara ya 8 wawili hao kukutana kwenye michuano hiyo, Chelsea ikimfunga Atletico Madrid mara 3, ikipoteza miwili na kutoa sare michezo miwili huku Atletico akiwa na rekodi nzuri ya kutokupoteza michezo yake kwenye uwanja wa Stamford Bridge chini ya Diego Simeone.
Mshindi wa jumla kati ya Chelsea na Atletico Madrid ataungana na aidha Bayern Munich au Lazio, Real Madrid ya Hispania, Borussia Dortmund ya Ujerumani, FC Porto ya Ureno, PSG ya Ufaransa, Manchester City na Liverpool zote za England kutinga hatua ya robo fainali.
Droo ya nani kucheza na nani kwenye hatua ya robo fainali pamoja na ile ya nusu fainali inatazamiwa kupangwa siku ya Ijumaa ya tarehe 19 Machi 2021 nchni Uswizi.