Thursday , 18th Mar , 2021

Mwanasheria na Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile, ameeleza mchango mkubwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe  Magufuli, katika sekta ya habari kuwa ni kuhakikisha uandishi wa habari unakuwa na viwango.

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile, Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe  Magufuli

Akizungumza katika Kipindi Maalum cha maombolezo ya siku 14 cha EATV Balile amesema Taifa la Tanzania limepoteza si tu kiongozi bali mtu muhimu aliyekuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya habari .

“Kama alivyoweka viwango kwenye taaluma nyingine na uandishi wa habari alilenga kuhakikisha  unakuwa na viwango ambavyo vinakubalika kuna watu walizoea kuandika uzushi, lakini baada ya kuhakikisha tunarudi kwenye misingi ya sheria ukipata habari anayetuhumiwa lazima apewe nafasi utafute vidokeze ili uandike  habari tukajikuta baadhi ya watu wanaotaka kuandika habari za harakaharaka  wakajikuta kwamba hawezi” amesema Balile

Awali akizungumzia mchango wa Rais Magufuli katika taaluma ya uandishi wa habari alisema miaka ya nyuma mtu yeyote ambaye alijua kusoma na kuandika aliona anaweza kuwa muandishi wa habari hivyo kusababisha kuwepo na wimbi la waandishi wasio kuwa na taaluma hiyo.