
Mshambuliaji nyota wa Brooklyn Nets, Kevin Durrant.
Nash amesema “Tunafuatilia hali yake na tunataraji atakuwa sawa hivi karibuni. Na tunaimani haitokuwa muda mrefu sana, lakini bila shaka anahitaji wiki mbili kujiweka sawa kabla hajarejea uwanjani”.
Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho mara ya mwisho Durrant kucheza mchezo na timu yke ya Brooklyn Nets ni Febrauri 15, 2021 lakini tokea kukosekana kwake, nyota James Harden na Kyrie Iriving wameweza kuonesha kiwango kizuri kwa kushinda michezo 11 na kupoteza mmoja pekee na kuwafanya kupanda hadi kuwa vinara wa upande wa Mashariki.
Brooklyn Nets inataraji kushuka dimbani saa 9:00 usiku wa kuamkia kesho tarehe 20 Machi 2021 kukipiga na Orlando Magic kwenye muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya kikapu nchini Marekani 'NBA'.