
Hayati Dkt. John Magufuli, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kauli hiyo ameitoa leo Machi 23, 2021, visiwani Zanzibar, wakati akivishukuru vyombo vya habari mbalimbali ambavyo vimejitoa kurusha mubashara shughuli zote za kuaga mwili wa Hayati Dkt. Magufuli.
"Nashukuru vyombo vya habari na kwa kweli mmekua nasi tangu siku ya kwanza hata tukio hili mnalirusha duniani kote, mpaka jana jioni tunazo taarifa waliofuatilia tukio la kuaga mwili wa Hayati Dkt. Magufuli, kitaifa jana Dodoma ni watu karibu bilioni 4, walikuwa wanafuatilia tukio la kuaga kwa mpendwa wetu," amesema Waziri Mkuu Majaliwa.