Wednesday , 24th Mar , 2021

Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli, umewasili Chato jioni ya leo Machi 24, 2021.

Mwili wakati ukiingizwa ndani

Msafara uliobeba mwili huo wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli ulianzia Mwanza baada ya wakazi wa mkoa huo na mikoa ya jirani kuuaga.

Kabla ya kufika Chato umepita wilaya za Misungwi katika eneo la Busisi kisha kuingia Sengerema, Geita, mji mdogo wa Katoro kisha Bwanga na jioni ukafika nyumbani kwao kijiji cha Mlimani wilaya ya Chato.

Wakazi wa Chato na maeneo ya jirani watapata nafasi ya kuaga siku ya kesho Alhamisi Machi 25, 2021 kabla ya mazishi kufanyika Ijumaa Machi 26, 2021.