Friday , 26th Mar , 2021

Kuelekea mazishi ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewashukuru wote walioshiriki tangu kifo mpaka sasa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Leo tunapompumzisha mpendwa wetu Hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwenye nyumba yake ya milele, kwa niaba yangu binafsi na niaba ya Watu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda kuwashukuru Watanzania wenzangu.

Viongozi wenzangu pamoja na Viongozi Wastaafu, Viongozi wa Nchi na Mashirika Mbalimbali ya Kimataifa, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Kisiasa, Jumuiya ya Kidiplomasia, Vyombo vya Habari, wasanii na kila aliyekuwa nasi bega kwa bega wakati huu mgumu kwa Taifa letu. 

Tafadhali pokeeni shukrani zetu za dhati na muendelee kuiombea roho ya Hayati Dkt. Magufuli ipumzike kwa amani na Mungu aendelee kuifariji familia yake.