Friday , 2nd Apr , 2021

Klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani imemwambia wakala wa mshambuliaji wa timu hiyo Erling Haaland Mino Raiola kuwa mchezaji huyo hauzwi kwa sasa. Lakini hali hiyo inaweza kubadilika endapo kama klabu hiyo haita shiriki ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao.

Erling Haaland

Raiola ameshaanza kufanya mazungumzo na baadhi ya vilabu barani ulaya ikiwa ni sehemu ya kumtaftia timu mteja wake huyo, ambapo wakala huyo ameongozana na baba mzazi wa Haaland Alf-Inge, wawili hao jana walikuwa nchini Hispania na kwa mujibu wa taarifa ni kwamba walifanya mazungumzo na vilabu viwili Real Madrid na FC Barcelona na hii leo wanaelekea nchini England ambako watafanya mazungumzo na vilabu vya Chelsea, Liverpool Manchester United na Manchester City.

Lakini mkurugenzi wa ufundi wa Dortmund Michael Zorc amesema kuwa wamemwambia Raiola kuwa hawana mpango wa kumuuza Haaland mwishoni mwa msimu huu,

''Nilizungumza na Raiola Jana Jumatano. Tulimweleza nia yetu, kuwa tuna mipango ya muda mrefu na Erling, na sio lazima azishugulikie uvumi. Nina muona akiwa nasi kwa muda mrefu zaidi'' amesema Michael Zorc

Mshambuliaji huyo Raia wa Norway mwenye umri wa miaka 20 anatajwa kuwa na thamani ya pouni milion 154 ambayo ni zaidi ya bilioni 494 kwqa pesa za kitanzania, na msimu huu amefunga mabao 33 kwenye michezo 31 kwenye michuano yote.