
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola (kushoto) akimpongeza mchezaji wake Sergio Aguero (kulia).
Guardiola amesema “Tuna wachezaji wakutosha kwa sasa kwenye timu kwasasa na tuna wachezaji wazuri kwenye timu ya vijana, kwa upande mwingine kuna nafasi kubwa ya kutosajili mshambuliaji mpya msimu ujao kutokana na hali ya uchumi ya Dunia kwasasa”.
Hayo yamekuja baaad ya Manchester City kuhusishwa na kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortrmund ya Ujerumani mwenye umri wa miaka 20 na uwezo wa hali ya juu wa ufumania nyavu kwani ameshatupia mabao 33 na kutengeneza mabao 8 kwenye michezo 31 katika michuano yote.
Haaland anaelezwa kuwa na thamani ya paundi milioni 100 za England ambazo ni sawa na shilingi bilioni 320 na zaidi ya milioni 451 za kitanzania.
(Mshambuliaji wa Dortmund, Erling Haaland.)
Guardiola ameendelea kwa kusema, “Kwa bei hizi hatuto sajili mshambuliaji yeyote. Haiwezekani, hatuwezi kugaharamia. Hilo halitotokea. Vilabu vyote vina haha na uchumi na sisi ni miongoni mwao.”
“Tuna Gabriel Jesus, tuna Ferran Torres ambao wamecheza vizuri sana kwenye nafasi hiyo, tuna wachezaji kwenye timu ya vijana na tumecheza mara nyingi na mshambuliaji kivuli.”
“Sijui nini kitakuja kutokea, huenda kikatokea, lakini huenda tusisajili mshambuliaji kwa msimu ujao.” Guardiola amesema.