Thursday , 15th Apr , 2021

Mbunge nje ya Bunge na msanii wa mkongwe wa muziki wa HipHop hapa nchini Prof Jay ameshea stori ya kile kilichotokea kati yake na Chidi Benz ambapo stori zilizotoka zilidai kwamba Prof Jay amepigwa na Chidi Benz.

Msanii Prof Jay akiwa kwenye studio za East Africa Radio

Prof Jay amekanusha stori hizo kwa kusema hakupigwa na Chidi Benz bali alisukumizwa mbele ya watu wake hali ambayo kama angesema arudishe basi Chidi Benzi angetoboka kama neti, pia Prof Jay amesema kitendo hicho alichofanya Chidi Benz ilikuwa kama amenyea kambi.

"Chidi Benz ni mdogo wangu kabisa, nimemtengeneza na alikuwa backstage wangu, aliletwa kwangu na Black Rhyno ila watu walimlisha madini hivyo akanyea kambi, hakunipiga ila alini-push kwenye mazingira magumu sana, nilikuwa na watu wangu kama ningesema wan'gate basi angekuwa na matobo kama neti, Chidi hawezi kunipiga hata tukiweka goma mbili" ameeleza Prof Jay

Kwa sasa Prof Jay amerudi rasmi kwenye muziki baada ya kipindi kirefu ambacho alikuwa anatumikia kazi ya wananchi wake wa Jimbo la Mikumi alipokuwa Mbunge.