Thursday , 15th Apr , 2021

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Kundo Mathew amesema serikali inaagalia namana inaweza kuleta uwiano kati ya watumiaji wa huduma, serikali na watoaji wa huduma katika suala zima la kushusha vifurushi vya mawasiliano kwenye simu.

Kushoto ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Kundo Mathew, Kulia

Mh. Kundo amesema hayo leo Bungeni, wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa jimbo la Kilolo, Justine Nyamoga kuhusu lini serikali itarudia mpango wake wa awali wa kushusha vifurushi ili Watanzania waweze kufurahia bei nafuu ya vifurushi.

"Changamoto ya biashara ya mawasiliano, kitu tunachoangalia serikali tunabalance namna gani kati ya watumiaji wa huduma, serikali na watoa huduma lazima tuangalie production cost (gharama za uzalishaji) ni lazima mwekezaji aweze kufanya biashara katika kiwango ambacho anaweza kupata faida ili serikali iweze kupata kodi ambazo zitasaidia kuleta maendeleo," Naibu Waziri Kundo amesema.

Awali akijibu swali bungeni Mh. Kundo amesema kwa sasa serikali ilijikita katika kuhakikisha bei za vifurushi zinarudi kwenye bei za awali kwani changamoto iliyokuwepo ni makampuni yalikuwa yana bei tofauti ambazo ziliwaumiza wananchi.