Monday , 19th Apr , 2021

Klabu za Chelsea na Leicester City watakutana katika mchezo wa fainali ya kombe la FA katika uwanja wa Wembley 15/05/2021.

Kelechi Iheanacho akishangilia goli alilofunga

Chelsea inayonolewa na kocha Mjerumani Thomas Tuchel ilitinga katika hatua hii siku ya jumamosi baada ya kuifunga timu ngumu ya Manchester City bao 1-0, goli lililofungwa na Hakim Ziyech, kunako dakika ya 55 ya mchezo kufuatia pasi ya Timo Warner.

Leicester City wao walifuzu siku ya jumapili baada ya kuifunga Southampton bao 1-0 goli lililofungwa na Kelechi Iheanacho dakika 55 kufuatia pasi ya mshambuliaji wao mahiri Jamie Vardy, kuambaamba na mpira pembeni mwa uwanja na kutoa pasi nzuri kwa mfungaji.

Leicester inayonolewa na Brandan Rogers, imeingia hatua hii kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1969 ilipofanya hivyo, mabingwa hawa wa EPL wa msimu wa mwaka 2015/16 watapaswa kupambana sana ili kutwaa ubingwa huo kwa kuwa kwa sasa Chelsea ndiyo inajengwa.

Takwimu zinaonesha Arsenal ndiyo timu wenye mafanikio zaidi kwa kutwaa ubingwa mara 14 katika fainali 21 alizocheza, Leicester City ndiyo inayoongoza kwa kucheza fainali nyingi bila kutwaa ubingwa wakiwa wamecheza mara 4 (1949,1961,1963 na 1963) sijui msimu huu itakuwaje?.