Monday , 19th Apr , 2021

Mcheza kikapu nyota wa timu ya Brooklyn Nets, Kevin Durrant amepata maumivu ya misuli jambo linalowapagawisha Nets kwani nyota wake Kyrie Iriving anahaha kurejea kwenye utimamu wake ilahli James Harden ana majeraha pia.

Nyota wa Brooklyn Nets, Kevin Durrant.

Durrant alipata maumivu hayo Jumapili ya jana Aprili 18, 2021 akiwa dimbani kucheza dhidi ya Makamu bingwa wa NBA, Miami Heat na Nets kupoteza mchezo huo kwa alama 109-107.

Kocha wa Nets, Steve Nash amesema, “Tutaona ataendeleaje baada ya kuamka, ila kwasasa hakuna kilichobainika juu ya maumivu yake. Tunategemea leo watamchunguza na kuangalia hali ya maumivu yake”.

Hii si mara ya kwanza kwa Durrant kupata maumivu hayo, kwani tayari ameshakosa michezo 33, 24 ni kutokana na maumivu ya misuli huku 6 ni kutokana na utaratibu za kiafya za kujikinga na Covid-19 na michezo mitatu mingine ni kutokana na majerah amengine ya kawaida.

Nae kocha wa Nets amejigamba kuwa wana wachezaji wengi vijana wa kuchukua nafasi hizo kuelekea michezo inayofuata.

NBA inatazamiwa kuendelea tena usiku wa kuamkia kesho kwa michezo 9, Philadelphia 76ers watakipiga na Golden State Warriors saa 8:30 usiku wa kuamkia kesho, Miami Heat na Houston Rockest saa 9:00 usiku ilhali LA Lakers watachuana na vinara wa upande wa mashariki Utaj Jazz saa 11:00 alfajiri.