Tuesday , 20th Apr , 2021

Wawakilishi wa nchi katika michuano ya Wavu klabu bingwa Africa MTC kutoka Mwanza ,wapo katika hatua nzuri kufuzu hatua ya robo fainali baada ya kufanikiwa kushinda seti 3-1 dhidi ya Wolaita Dicha ya Ethiopia

kikosi cha MTC kinachopeperusha bendera vyema Tunisia

Ushindi unaowafanya kuwa na alama 4 baada ya mchezo wa kwanza kupata alama moja inayotokana na kupata seti 2 katika mchezo wa kwanza licha ya kupoteza kwa seti 3-2

Majaliwa yawa MTC yapo katika mchezo wa leo kwenye dhidi ya wenyeji Olymipic Kalebia wanaoongoza kundi hilo ambapo itatoa hatma japo mazingira yake si mabaya kwa kuwa wanahitajika hata kama watapotez a basi wapate angalao seti 2 ili waweze kupata alama 1 itakayowafanya kufuzu

Michuano hiyo iliyoanza tarehe 18-4-2021 inatarajiwa kumalizika 28-4-2021 inashirikisha timu ishirini zilizopo kwenye makundi, inaonekana kufanikiwa sana kutokana na ushindani uliopo

Licha ya MTC kufanya vyema hadi sasa lakini mafanikio mengine kwa Watanzania yapo kwa mwamuzi wa kimataifa anayechezesha michuano hiyo Alfred Selengia ambaye alichezesha vizuri mechi KPA ya Kenya na APR ya Rwanda

Hadi sasa msimamo wa kundi upo kama ufuatavyo

1 Olympic Kalebia 6

2 . MTC 4

3 Nemo 2

4 Dicha 0