Friday , 23rd Apr , 2021

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp na kiungo wa kati wa Manchester City, Ikay Gundogan wameligeukia shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA kwa kuja na wazo na kutaka kubadilisha mfumo wa michuano hiyo jambo litakalo pelekea kuongezeka kwa idadi ya michezo itakayochosha zaidi wachezaji.

Kiungo wa Manchester City, Ilkay Gundogan (kushoto) na kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp (kulia).

Gundogan amesema hayo usiku wa kuamkia leo kupitia ukurasa wake wa twitter akitaka Afya za wachezaji zifikiriwe na kupewa kipaumbele wakati shirikisho la soka barani humo linavyotaka kubadili mfumo wa uchezaji wa michuano hiyo na kuongeza michezo kutoka 125 hadi 225.

Gundogan ameandika, “Kwa yote yanayoendelea kuhusu European Supe Ligi, tafadhali tuzungumzie mfumo mpya wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya. Michezo mingi  sana, hayupo hata mmoja anayetufikiria sisi wachezaji”.

“Mfumo mpya wa ligi ya mabingwa Ulaya ni ya kiwango cha chini sawa na ukilinganisha na European Super Ligi.”
Gundogan ametamani mfumo uliopo wa sasa wa michuano hiyo usalie kama ulivyo kwani upo vizuri na ndiyo maana unafanya michuano hiyo kuwa maarufu Ulimwenguni.

“Mfumo uliopo kwa sasas unafanyakazi vizuri na ndiyo maana ni michuano maarufu zaidi Duniani kwa ngazi ya vilabu, kwetu sisi na kwa mashabiki wetu”

Alichokisema Gundogan hakipishani na alichosema kocha wake wa zamani, Jurgen Klopp ambaye kwa sasa ni kocha wa Liverpool ya England. Klopp alisema hapendi kuona mfumo mpya wa michuano ya UEFA ikibadilika kwasababu kutakuwa na michezo mingi sana.

“UEFA walinionesha mfumo mpya, nilisema siupendi miezi kadhaa iliyopita, kwasababu ya kuwa na michezo mingi. Sitegemei wasifanye kwasababu nimesema siipendi lakini itakuwa na michezo mingi sana”.

Ikumbukwe kuwa mfumo huo mpya wa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, upo kwenye majadiliano huku ikitazamiwa kuanza msimu wa mwaka 2024-2025 kama ukipitishwa.