Friday , 23rd Apr , 2021

Wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya klabu bingwa ya mpira wa wavu Africa MTC kutoka Mwanza jana walishinda mchezo wao dhidi Societe Omnisport de Armie ya Cameroon, katika robo fainali ya kundi la pili isiyotoa ubingwa.

Wachezaji wa MTC wakishangilia ushindi

MTC ilitoa kichapo cha seti 3-0 dhidi ya Societe Omnisport de Armie na kujiahakikishi kumaliza katika nafasi ya 9-12 miongoni mwa timu 16 zilizoshiriki, hii inatokana na kushindwa kuingia katika robo fainali ya kwanza inayotoa bingwa kutoka makundi manne ya awali

Muundo wa mashindano kuna jumla ya timu 16 zilizokuwa katika makundi 4 vinara wa makundi na wale walioshika nafasi za 2 katika kila kundi wanakwenda kwenye robo fainali ya kwanza (1-8) inayotoa bigwa, robo fainali ya pili inahusisha timu ya (9-16) isiyotoa bingwa ila itasaidia kupanga nafasi ya kila timu toka 1-16

Michuano hiyo mikongwe ya mpira wa wavu Africa, inayofanyika Tunisia ilianza tarehe 18/04/2021 na inatazamiwa kumalizia tarehe 28/04/2021 kwa kumpata bingwa wake