Saturday , 24th Apr , 2021

Lulu Diva amenyoosha maelezo kuhusu kupata comments za baadhi ya mashabiki mitandaoni ambao wanaushambulia sana muonekano wake kwamba anatumia mkorogo na kujichubua.

Msanii Lulu Diva

Akijibu hilo kupitia Kamera za EATV & EA Radio Digital, msanii Lulu Diva amesema suala la muonekano wake hayawahusu mashabiki kwa sababu ni mambo yake binafsi ila wanachotakiwa ni kuangalia kazi zake.

"Suala la muonekano wangu ni wangu na ipo 'very personal' hata nikitaka kuwa mwembamba nitakuwa nimeamua mwenyewe kwa sababu hata shabiki naye ana mwili wake, kama wanahisi hivyo 'it's okay' siwezi kukaa kuanza kujielezea kwamba sipaki lotion au kuna vitamins natumia ili kuwa mweupe" ameeleza Lulu Diva

Mengi zaidi aliyoyazungumza kuhusu tuhuma za kujichubua bonyeza hapa chini kutazama.