Saturday , 24th Apr , 2021

Mwenyekiti wa Klabu ya Simba,Murtaza Mangungu amesema licha ya Mtendaji Mkuu wao, Barbra Gonzalez kukutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Innocent Bashungwa kujadili mambo mbalimbali kuhusu mchakato wao wa mabadiliko ya uendeshaji wa Klabu yao, bado hawana mamlaka ya

Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu akizungumza na Wanachama wa Klabu hiyo katika mkutano Mkuu.

Kauli hiyo imekuja baada ya Mangungu kuulizwa na East Africa Radio kuhusu ni hatua ipi wamefikia kufuatia kuwepo kwa taarifa zenye mkang'anyiko juu ya mchakato wao wa mabadiliko ya uendeshwaji wa wekundu wa msimbazi Simba, ambapo idadaiwa kuna sehemu unakwamishwa.

Hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii ya Muwekezaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohamed Dewji aliandika kwamba anasikitishwa kwamba licha ya kukutana na kufanya mazungumzo na Tume ya ushindani na kukaribia kufikia tamati lakini walipokea barua iliyowaamuru waanze upya mchakato wa mabadiliko jambo ambalo anaamini litawachelewesha kufikia malengo.

Kufuatia taharuki hiyo mitandaoni, Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba alionekana akiwa na Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mh Innocent Bashungwa kujadili masuala kadhaa likiwemo hili la mkwamo wa mchakato wa mabadiliko ya uendeshwaji wa timu hiyo ambapo iliarifiwa pande hizo mbili zingekutana Jumatatu iliyopita kutatua changamoto zilizopo.

Hata hivyo Mwenyekiti Mangungu amesema kwa sasa nyota wa mchezo ni FCC na wao ndio kilakitu hivyo taarifa yoyote itatolewa na wao mpaka pale na wao watakapokuwa na mamlaka ya kuzungumza na Umma.