
Moja ya picha za satelite za kimbunga Jobo kutoka TMA
Taarifa ya TMA imeeleza kuwa nguvu ya kimbunga Jobo imepotea wakati kikiingia nchi kavu kusini mwa mkoa wa Pwani na Dar Es Salaam usiku wa tarehe 24/04/2021.
Hali hii ilisababishwa na kuendelea kuimarika kwa upepo baharini karibu na maeneo ya kusini mwa pwani ya Tanzania na Msumbiji.
Hivyo kwa sasa, kimbunga Jobo hakipo tena nchini Tanzania na hakuna madhara ya moja kwa moja yanayotarajiwa.