Mbinu hii mpya kuvutia uwekezaji nchini

Wednesday , 12th May , 2021

Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Prof. Godius Kahyarara amesema uzinduzi wa Kituo Cha huduma kwa wateja utapunguza gharama na mizunguko kwa wawekezaji ambao wamekuwa wakifika hapa nchini.

Kulia Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Prof Godius Kahyarara, Kushoto ni Kituo cha Uwekezaji Tanzania

Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kuzindua Kituo hicho Cha huduma kwa wateja kilichopo katika Kituo Cha Uwekezaji Nchini Tanzania TIC ambapo amesema kwa kipindi chote sasa kupitia Kituo hicho wawekezaji watapata nafasi ya kupata taarifa zote za kiuwekezaji kupitia simu.

"Sasa hivi uwepo wa Kituo hiki Cha huduma kwa wateja kitawasaidia wenye uhitaji wa kuwekeza kupata taarifa sahihi wakati wote hii pia ikipunguza gharama na muda wa wawekezaji kuzunguka" amesema Prof. Kahyarara

Aidha amesema kuwa awali Kituo hicho hakikuwepo lakini kutokana na nia ya serikali ya kuongeza wawekezaji imelazimika kufungua Kituo hicho ili kuhakikisha wawekezaji wanapatiwa huduma stahiki kwa wakati.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa sekta binafsi idara ya wanachama Zaki Mbena amesema Wawekezaji wanapenda mazingira rafiki kama hayo.