Thursday , 24th Jun , 2021

Bingwa mtetezi mara mbili, Andy Murray amejumuishwa katika kikosi cha timu ya Uingereza ya mchezo wa Tenisi itakayoshiriki katika michuano ya Olimpiki mwaka huu.

Muingereza Andy Murray akionesha makeke yake uwanjani

Murray mwenye umri wa miaka 34 atacheza pamoja na Dan Evance kwenye michuano ya mmoja mmoja pia ataambatana na Joe Salisbury kwenye mechi zinazohusisha watu wawili.

Hakuna nafasi kwa mbabe wa mechi za washiriki wawili wawili, Jammie Murray kwenye timu hiyo, ingawa Heather Watson na Johana Konta watawakilisha kwa upande wa timu ya wanawake.

Mashindano ya Olimpiki yalipaswa kufanyika mwaka jana lakini yaliahirishwa kufuatia janga la ugonjwa wa Covid-19.