Thursday , 24th Jun , 2021

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amewataka Wakazi wa Dar es Salaam kuchukua tahadhari dhidi ya mlipuko wa wimbi la tatu la virusi vya corona ikiwemo kuzingatia uvaaji sahihi wa barakoa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla (Watatu kulia)

Bw. Makalla amesema hayo Jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza kutokana na jiografia ya mkoa wa Dar es Salaam kuwa nyeti na unapokea wageni kutoka ndani na nje ya nchi wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari zakutosha.

“Naomba tuchukue tahadhari moja ni kuvaa kwa usahihi barakoa kila wakati katika sehemu zeneye mikusanyiko ya watu wengi kama kwenye vyombo vya usafiri na vituo vyake kwenye masoko katika sherehe, nyumba za ibada vituo vya faya maofisini,” amesema Bw. Makalla.

Pia Bw. Makalla amesema mwananchi yeyote akiona dalili zinazofanana na dalili za virusi hivyo kuwahi hospitalini kwa ajili ya vipimo.

Tahadhari hii inakuja kufuatia taarifa kutoka Wizara ya Afya, juu ya uwezekano wa kutokea kwa wimbi la maambukizi ya Covid-19 ambayo yanakabili nchi nyingine hivyo kutahadhirisha umma kuendelea kuchukua tahadhari na kuzingatia taarifa zinazotolewa.