Wachezaji wa Simba
KMC ndio wenyeji wa mchezo huu na wanaingia kwenye mchezo wa usiku wa leo wakiwa na rekodi mbaya dhidi ya Simba kwenye michezo ya Ligi Kuu, ambapo takwimu zinaonyesha katika michezo mitano ya ligi waliokutana Simba wameshinda michezo yote.
Lakini pia timu hiyo kutoka Manispaa ya kinondoni haijawa na mwenendo mzuri kwani katika michezo yao mitano ya mwisho wamefungwa michezo miwili na wametoka sare michezo mitatu hivyo hawajashindi mchezo hata mmoja. KMC wapo nafasi 6 wakiwa na alama 42 katika michezo 31.
Simba wanahitaji alama nne (4) kwenye michezo minne ya Ligi iliyosalia ilikutangazwa mabingwa wa Ligi Kuu kwa msimu wanne mfululizo kwa sasa wana alama 73 wakiwa ndio vinara na endapo kama wakishinda mchezo wa leo basi itabaki alama moja tu kuwa mabingwa wa VPL.






