Mwenyekiti wa Yanga, Dokta Mshindo Msola akizungumza katika moja ya Mkutano na Waandishi wa Habari
Yanga na Azam watashirikiana kuandaa na kuyarusha maudhui ya klabu hiyo ikiwemo Mazoezi, maandalizi ya mechi, michezo ya kimataifa lengo likiwa ni kuhakikisha wanachama na mashabiki wa klabu hiyo watakuwa wanapokea taarifa zao kwa wakati.
Kuanzia msimu ujao,Kila Mwezi Yanga itakuwa ikilipwa Milioni 200 kila mwezi na Azam Media kupitia Mkataba huo maana yake watachukua Bilioni 2.4 kwa mwaka.
Kiasi cha fedha kitaendelea kuongezeka kila mwaka kutokana na makubaliano yaliyoafikiana.




