Wednesday , 18th Aug , 2021

Nguli wa zamani wa klabu ya Arsenal Paul Merson amekosoa sera ya usajili ya klabu yake hiyo ya zamani akisema wamekuwa wanafanya usajili wakawaida huku akimkosoa mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo Edu akisisitiza usajili unaofanyika unamuacha nyuma kocha Mikel Arteta.

Edu (kushoto) mkurugenzi wa ufundi wa Arsenal akiwa na kocha Mikel Arteta.

Gwiji huyo amesema hayo kufuatia Arsenal kufungwa kwanye mchezo wa kwanza wa Ligi dhidi ya Brentford kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu England msimu wa 2021-22, huku akisisitiza kilichotokea kilikuwa kinategemea na kilitabiliwa tangu awali.

 

''Inatia wasiwasi Arsenal, bado unafikiria wanaenda wapi? Edu ameingia, na usajiri umekuwa wakivivu, nikiwa mkweli imekuwa ni "Ah, tutamchukua Willian bure… tutamchukua David Luiz kwa bei rahisi. Nakumbuka miaka iliyopita katika mpira wa miguu, mameneja walihukumiwa kwa usajili. Wakati mwingine nadhani Arteta ameachwa nyuma, na sina hakika ni kiasi gani cha kusema amepata katika haya yote.'' Amesema Paul Merson

 

Paul Merson aliichezea Arsenal zaidi ya michezo 423 kwenye michuano yote kati ya mwaka 1985 hadi 1995 katika nafasi ya ushambuliaji na alishinda jumla ya mataji saba (7) ukiwemo ubingwa wa England mara 2 msimu wa 1988-89 na 1990-91.

Paul Merson

 

Katika dirisha hili la usajili Arsenal imewasajili wachezaji watatu wa kikosi cha kwanza mpaka sasa ambao ni Ben White kutoka Brighton & Hove Albion, Nuno Tavares kutoka Benifica, Albert Sambi Lokonga kutoka Anderlecht na masaa machache yajayo wanaweza kumtangaza kiungo mshambuliaji Martin Ordegaard kuwa mchezaji mpya wa kikosi hicho akitokea kutoka Real Madrid.