Thursday , 19th Aug , 2021

Bingwa mtetezi wa michuano ya tennisi ya US Open, Dominic Thiem raia wa Australia atakosekana kwenye michuano hiyo inayotaraji kufanyika Agosti 30 mwaka huu nchini Marekani kutokana na nyota huyo kujitonesha mkono wake siku ya jana alipojaribu kufanya mazoezi mepesi.

Mcheza tennisi wa sita kwa ubora duniani kwa wanaume, Dominic Thiem.

Thiem ambaye anashikilia nafasi ya sita kwenye viwango vya ubora vya tenisi duniani kwa wanaume, amesema uamuzi wa kukosekana kwenye michuano hiyo umekuja baada ya ushauri aliopewa na jopo la madaktari wake na kuthibitisha nyota huyo atakuwa nje kwa mwaka mzima.

Mara ya mwisho Thiem kujitupa dimbani ilikuwa ni mwezi Juni mwaka huu kwenye michezo ya Mallorca Open nchini Hispania ambapo alipata maumivu hayo ya mkono.