
Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili nchini (BAKITA) Oni Sigalla,
Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 20, 2021, kwenye mjadala uliohoji iwapo jamii inaridhishwa na maudhui ya muziki wa kizazi kipya, ulioendeshwa na kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio.
"Leo hii vijana wetu (Wasanii) mniwie radhi, sasa wamekuwa na Benki ndogo sana ya misamiati, hana mbadala wala uwezo wa kufikiria kwamba hili ninaweza kuzunguka kona hii nikaamiaanisha hivi wao wanaenda na njia ya mkato moja kwa moja," amesema Oni Sigalla
Aidha, ameongeza kuwa, "Uwezo wa mtu kuzungumza ndiyo ukomo wa akili yake, tunadhani wasanii wetu baadhi wamefikia mahali ambapo wanadhani muziki ni sehemu pekee ambako anaweza kujimwayamwaya na matusi na anaweza kuzungumzia jambo lolote baya".