
Picha ya pamoja ya wachezaji Vincent Kompany na David Silva
Man City wamefanya hivyo kama sehemu ya kutambua mchango wao kwenye klabu huku wawili hao kwa pamoja wakiwa wameitumikia na kuipatia mafanikio makubwa kama kushinda mataji ya Ligi Kuu, FA na EFL tangu walipojiunga kabla ya kuondoka.
Kompany alichezea City kwa misimu 11 na akiwa kama nahodha alifanikiwa kuiongoza klabu hiyo kutwaa taji la kwanza la Ligi Kuu baada ya miaka 44 kupita msimu wa 2011/12 ambapo pia walifanikiwa kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu huo kwa mara ya kwanza.
Klabu hiyo bado ipo kwenye ujenzi wa sanamu la tatu la Sergio Aguero ambalo linatarajiwa kukamilika mwakani.
Kompany na Silva waliondoka Manchester City mwezi Juni 2019.