Sunday , 29th Aug , 2021

Tume ya Tehama Tanzania imekusudia kukusanya na kuyaendeleza mawazo ya kiteknolojia kutoka kwa watu mbalimbali watakaojisajili kupitia mfumo maalum (Soft Center) ikilenga kuhamasisha zaidi maeneo muhimu zaidi kwa wawekezaji kuja na kuwekeza kupitia teknolojia ya Tehama.

Mkurugenzi Tume ya Tehama Samson Mwela (aliyesimama) akitoa mafunzo maalum kwa watangazaji na waandishi kutoka kituo cha East Africa Television na East Africa Radio.

Mkurugenzi Tume ya Tehama Samson Mwela, ameeleza hilo wakati akitoa mafunzo maalum kwa watangazaji na waandishi kutoka kituo cha East Africa Television na East Africa Radio.

Aidha ameongeza kuwa kwa sasa bado takwimu zinaonyesha eneo hili la Tehama bado watu hawajalitumia ipasavyo licha ya kwamba kwa sasa dunia iko katika ulimwengu huo.

Namna ya kushiriki tuzo za Tehama (ICT Awards 2021) bonyeza hapa 

Tazama video hacpo chini