Tuesday , 31st Aug , 2021

Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela leo Agosti 31, 2021 amemtangaza, Senzo Mbatha raia wa Afrika Kusini, kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo.

Senzo Mbatha

Kwa majukumu hayo ana jukumu la kusimamia mchakato wa mabadiliko kufikia mwisho na aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Haji Mfikirwa atakuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.

Fredrick Mwakalebela ametangaza hayo baada ya Katiba ya Yanga kubadilishwa baada ya wanachama wa klabu hiyo kupitisha mchakato wa mabadiliko kwa asilimia mia moja.

Mbatha awali alikuwa mshauri mkuu wa Yanga kuelekea kwenye mabadiliko baada ya kubwaga manyanga ndani ya Simba SC ambapo alikuwa kwenye nafasi hiyo.

Ndani ya Yanga anakuwa ni Mtendaji Mkuu wa mpito, (Interm CEO) wa klabu ya Yanga kufuatia utekelezwaji wa mfumo wa uendeshaji wa klabu.