
Msanii Mimi Mars
Mimi Mars amefunguka hilo kupitia kipindi cha Nirvana ya East Africa TV kinachoruka siku ya Jumanne kuanzia saa 3 kamili usiku akimzungumzia mwanaume aliyekuwa naye kwenye mahusiano.
"Kimuonekano ni mrefu mweusi ana utu na anampenda Mungu anapambana kutafuta huwezi kusema ana pesa sana yupo kati kati, Mimi siyo mwanamke wa kupenda kupewa pesa na mwanaume" amesema Mimi Mars
Baadhi ya wadau wameshea maoni yao kwa kuandika Mimi Mars apewe ulinzi au ajengewe sanamu kwa kutopenda pesa tofauti na baadhi ya wanawake wengine.