Wednesday , 1st Sep , 2021

Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, amewatoa hofu waliokuwa wakihofia kwamba ili uwekeze katika soko hilo inakubidi uwe na mtaji mkubwa kwa kusema kiwango cha mwisho cha uwekezaji wa hisa katika soko hilo ni hisa 10 tu na kila hisa moja inauzwa Tsh 200

Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba Mosi, 2021, wakati yeye na timu yake walipotembelea kwenye ofisi za Makampuni ya IPP Media, za magazeti ya The Guardian, East Africa Television na East Africa Radio, ITV na Radio One pamoja na Capital TV na Capital Radio, kwa lengo la kujifunza na kuona namna vyombo hivyo vinavyoendesha shughuli zake.

Mbali na hayo Moremi akauhakikishia uongozi wa makampuni ya IPP kwamba, kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam watahakikisha wanafanya kazi kwa ukaribu na Makampuni ya IPP Media, kwa lengo la kuhakikisha elimu ya masoko na mitaji ndani ya soko hilo inatolewa na kuwafikia wananchi walio wengi zaidi.