
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Hayo yamesema na Mwenyekiti wa Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Wallace Karia leo Jijini Nairobi nchini Kenya ambako mashindano ya mwaka huu yanendelea nchini Kenya.
Karia ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), amesema udhamini huo ni endelevu na kila mwaka Rais samia atatoa dola 100,000 kwa ajili ya mashindano hayo ambayo kuanzia leo yatajulikana kama CECAFA Womens Samia Cup.
Katika fedha hizo, bingwa ataibuka na kitita cha 30,000 USD sawa na milioni 65 na zaidi ya laki tano, mshindi wa pili dola 20,000 sawa na milioni 46 na zaidi ya laki tatu za kitanzania, mshindi watatu atapata dola 10,000 sawa na milioni 23 na zaidi ya laki moja za Kitanzania (itategemea na mabadiliko ya thamani ya dola) na fedha nyingine zitatumika kwa mambo mengine katika mashindano hayo ikiwemo kutoa zawadi za wachezaji na marefa bora.
Kwa mwaka huu, Simba Queens ndio inaiwakilisha Tanzania huko na baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya PVP FC ya Burundi na sare ya 0-0 na Lady Doves WFC ya Uganda – watakamilisha mechi zao za Kundi A kwa kumenyana na FAD FC ya Djibouti kesho Setpemba 2, 2021.
Bingwa atashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye mwaka huu nchini Misri ambayo itahusisha timu nane, nyingine kutoka kanda nyingine barani zitakazogawanywa katika makundi mawili.