Friday , 3rd Sep , 2021

Mshambuliaji wa Manchester United, Cristiano Ronaldo ameingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha  Guiness baada ya kufunga magoli 111 akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Ureno, akiwa amehudumu ndani ya timu ya taifa kwanzia mwaka 2003-2021.

Kumbukizi ya Cristiano Ronaldo akiwa anapokea cheti kutoka kitabu cha rekodi za Dunia cha Guiness baada ya kuweka rekodi kadhaa za kibabe.

Ronaldo alivunja rekodi ya ulimwengu ya mabao yaliyofungwa katika soka wakati alipofunga mabao yake 110 na 111 kwa Ureno katika ushindi wao wa kufuzu wa Kombe la Dunia wa mabao 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Ireland.

Baada ya kupewa tuzo hiyo Ronaldo alisema: ''Asante kwa Guiness World Records. Daima ni vizuri kutambuliwa kama mvunjaji rekodi wa ulimwengu. Wacha tuendelee kujaribu kuweka nambari zaidi''.

(Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo akiwa ameshikilia cheti kutoka kitabu cha rekodi za Dunia cha Guiness baada ya  kukabidhiwa usiku wa kuamkia leo kwa kufikisha mabao 111 na kuwa mchezaji pekee mwenye mabai mengi kwa upande wa timu za taifa.)

Mchezaji huyo mwenye miaka 36 kwasasa alifunga mabao mawili kwa kichwa dakika za lala salama na kuifikia na kuongeza rekodi licha ya kukosa penalti iliyookolewa na Gavin Bazunu.

Ali Daei, ambaye alifunga mabao 109 kwenye timu yake ya taifa ya Iran kati ya mwaka 1993 na 2006, na alishikilia rekodi hiyo ambayo Ronaldo alikuwa sawa naye ambaye aliigikia baada ya kufunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Ufaransa kwenye michuano ya Euros 2020.

Mshambuliaji huyo wa Manchester United pia amefikia rekodi ya Sergio Ramos wa timu ya taifa ya Hispania kwa kuwa na michezo mingi ya timu za taifa, michezo 180.