Monday , 6th Sep , 2021

Mchezaji wa zamani wa AC Milan na timu ya taifa ya Italia Alessandro Nesta amesema anaamini kikosi cha AC Milan kipo kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Italia Serie A msimu huu, licha ya timu hiyo kutopewa nafasi yakuwa mabingwa wa Scudetto.

Wachezaji wa kikosi cha AC Milan

Msimu uliopita AC Milan ilimaliza nafasi ya pili kwenye msimamo, alama 12 nyuma ya mabingwa na wapinzani wao kutoka katila Jiji la Milan Inter Milan ambao ndio walikuwa mabingwa. Na msimu huu wa 2021-22 Milan imeuanza msimu vizuri baada ya kushinda michezo yote miwili ya mwanzoni mwa msimu, ikiwa imekusanya alama zote  sita (6) na wapo nafasi ya nne (4) kwenye msimamo.

“AC Milan ni washindani wa ubingwa wa Ligi kuu Itallia (Scudetto). Labda wameanza msimu kama timu ambayo haipewi nafasi, lakini hilo sio jambo baya. Ukweli ni kwamba kuna timu nyingi ambazo zinaweza kushinda mwaka huu, Jambo moja ni wako kwenye njia sahihi." Amesema Alessandro Nesta juu

Beki huyo wa kati wa zamani Milan alishinda mataji 10 akiwa na kikosi hicho kati ya mwaka 2002 mpaka 2012, na mataji mawili kati ya hayo yalikuwa ya Ligi kuu nchini Italia na ubingwa wa klabu bingwa ulaya mara mbili. Nesta aliichezea Rossoneri jumla ya michezo 326 akifunga mabao 10 kwenye michuano yote.