
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi
Jaji Mutungi ameeleza hayo leo Jijini Dar es Salaam na kusema ameitisha mkutano huo ili kufanya mazungumzo na wadau hao muhimu ili kuondoa sintofahamu iliyoibuka baada ya kudaiwa polisi kuingilia na kuzuia mikutano ya kisiasa ya ndani.
Hatua hiyo imekuja baada ya siku za hivi karibuni Chama cha NCCR- Mageuzi kilinukuliwa kikilalamikia kuzuiwa na Jeshi la Polisi kufanya mkutano wa Kamati Kuu katika eneo la Msimbazi baada ya Polisi hao kuvamia mkutano huo