
George Russel
Russell anaondoka kwenye kampuni ya Williams baada ya kuitumikia kwa miaka Mitatu, huku msimu uliopita aliweka wazi kiu yake ya kujiunga na timu kubwa ambapo ataungana na Muingereza mwenzake Lewis Hamilton.
Akiwa na miaka 23, Russell ameonesha uwezo wa hali wa kuendesha magari ya Langalanga, akimaliza nafasi ya pili kwenye mashindano Belgium grand prix mwezi uliopita huku akiendesha moja ya magari yenye mwendo wa pole pole katika gridi.
Russell ataangaziwa kuwa mchezaji wa kwanza kumshinda Hamilton kama mchezaji mwenza wa timu moja ya Mercedes tangu Nico Rosberg afanye hivyo 2016.