
Kushoto ni Hayati Dkt John Magufuli na kulia ni Hayati Benjamin Mkapa
Waziri Mhagama ameeleza umuhimu wa ibada hiyo, kwa kuzingatia michango ya viongozi hao katika Taifa na kusema ni sehemu ya kuwaenzi na kuonesha heshima kwa namna walivyolitumikia Taifa.
Aliongezea kuwa, Kanisa kwa kushirikiana na kamati ya maandalizi wana jukumu la kuiandaa ibada hiyo ya kipekee kulingana na heshima kubwa ya viongozi hao katika Taifa na kuonesha tunatambua michango yao kwa matendo.
Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru 2021, zitahitimishwa Oktoba 14 wilayani Chato mkoani Geita.