Tuesday , 14th Sep , 2021

Mchungaji Deborah Kaisi amesema kuna baadhi ya wanaume hawajaandaliwa kuwa vicha vya famili na kwenye ndoa ndio maana wamekuwa wazembe wakisuburu kuoa wanawake wenye pesa.

Picha ya Mchungaji Deborah Kaisi

Akizungumzia hilo kwenye kipindi cha MamaMia ya East Africa Radio wakati wanajadili kuhusu masuala ya ndoa na majukumu Mchungaji Deborah Kaisi anasema.

"Baadhi ya watoto wa kiume hawajaandaliwa kuwa vichwa vya familia na kwenye ndoa, wengi wao wanasubiri kuwaoa wanawake wenye pesa, ndio maana wanaume wengi wamekuwa wazembe wazembe". 

Pia ameongeza kusema "Mungu alitengeneza ndoa kama raha na sio karaha, kusaidiana kiuchumi, pia mume akapewa jukumu na wajibu wa kulea mtoto na mke".