Wednesday , 15th Sep , 2021

Harmonize hachoki kupika kazi mpya kila siku, wakati akiendelea na tour yake Marekani ameingia studio kupika albamu mpya na mtayarishaji wa muziki Mr Simon kutoka nchini Norway.

Picha ya Msanii Harmonize na Producer Mr. Simon

Kupitia insta story yake ame-share video akiwa studio na mtayarishaji huyo huku akisikika akisema kuwa albamu ijayo  ambayo itakuwa ni ya tatu itaitwa “Arizona” kwasababu ameipika akiwa katika jimbo hilo linalopatikana katika mji mkuu wa Phoenix.

Taarifa zinasema albamu yake ya pili “High School” tayari imekamilika na kinachosubiriwa ni kuachiwa tu.