Thursday , 16th Sep , 2021

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. George Simbachawene, ameelekeza vyombo vyote vya ulinzi na usalama nchini kuwatafuta watu wote wanaowachafua wenzao mitandaoni hasa wanaomdhihaki Rais wa Tanzania na Serikali na hatua kali zifuatwe na kuwafikisha mahakamani kwa haraka.

Rais Samia Suluhu (kulia) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. George Simbachawene

Waziri Simbachawene ameyasema hayo mapema leo Alhamisi Jijini Dodoma wakati akizungimza na viongozi wa idara zote za ulinzi na usalama nchini ambapo ameelekeza kufanyike msako wa haraka kuwabaini watu hao na kuwakamata kwakua kumeibuka tabia ya watu kutumia vibaya mitandaoni hiyo kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza.

Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene ameagiza msako wa wezi mitandaoni kwa kuwa inakadiriwa kuwa kwa siku milioni 500 zinakua kwenye wizi wa kimatandao huku akikataza wananchi kutoa fedha kwa ajili yakufuatilia polisi taarifa za simu zao zilizoibiwa.