Monday , 20th Sep , 2021

Kutoka Weusi Kampuni mwanahiphop Joh Makini ni mmoja wa wasanii walioshambulia stage siku ya Simba Day uwanja Benjamin William Mkapa, Temeke Dar es Salaam.

Joh Makini akiperfome siku ya Simba Day

Kupitia show ya PlanetBongo ya East Africa Radio ameshea maoni yake baada ya kumalizika kwa tamasha hilo ambapo anasema.

"Najisikia vizuri kuwa sehemu ya historia barani Afrika nikiwa kama shabiki wa Simba, pia ni kitu kikubwa kwa muziki ninaoufanya maana Simba Day ni siku kubwa sana kupata nafasi ya kutumbuiza ni kama tumepata heshima mimi na muziki wa HipHop"

"Mpira uendelee kupewa nafasi, tuuheshimu na unaweza kubadilisha maisha ya watu wengi sana kwa sababu tukio kama la jana watu wameweza kupata kipato, wengine wametengeneza carrier za kutumiza ndoto zao ni kitu kizuri" ameongeza

Baadhi wa wasanii wengine walioperfome ni Prof Jay, Whozu, Saraphina, Meja Kunta na Marioo.