Tuesday , 5th Oct , 2021

Uongozi wa klabu ya Manchester united inafanya mazungumzo na makocha wake wasaidizi Michael Carrick na Kieran McKenna ili kuwaongezea mkataba wa miaka mitatu hadi mwaka 2021 kuendelea kuhudumia benchi lake la ufundi.

Makocha wasaidizi wa klabu ya Manchester United, Michael Carrick (kushoto) na Kieran MCkenna (kulia).

Taarifa hizo zimekuja siku chache baada ya Manchester united kumuongezea mkataba wa miaka mitatau kocha msaidizi nambari moja, Mike Phelan hadi mwaka 2024 ili aendelee kuijenga timu chini ya Ole Gunnar Solskjear.

Mazungumzo ya wasaidizi hayo yanaelezwa kwenda vizuri na muda wowote kuanzia leo Oktoba 5, 2021 Manchester United itathibitisha kuwasinisha kandarasi hizo makocha hao ambao walijiunga na United tokea Disemba 2018.

Kwa upande wa kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjear ambaye hajabeba taji hadi sasa, bado yupo yupo sana United hadi mwaka 2024 baada ya kusaini Kandarasi ya miaka mitatu Julai mwaka huu kuendelea kuijenga timu hiyo.

Ikumbukwe kuwa Solskjear na jopo lake la benchi la Ufundi liliingia kwa pamoja Disemba 2018 baada ya Jose Mourinho kufukwa kazi kufuatia soka lisiloridhisha licha ya kufanikiwa kubeba mataji ya UEFA EUROPA na Makombe ya FA.